alt text

Royal Jelly Capsule


Viungo:


Royal Jelly softgel 100% Natural Royal Jelly

Kazi Na Faida Zake



Yafaa Kutumika Kwa:


Maelezo Muhimu:


Royal jelly - "chakula chenye hadhi" cha malkia wa nyuki:
Royal jelly ndicho chakula maalumu cha malkia wa nyuki kwa maisha yake yote, chakula kinachochangia malkia huyu aishi maisha marefu ( mara 50 ya urefu wa maisha ya nyuki kijakazi ), na kuwa na uwezo wa kutaga mayai mengi. Malkia wa nyuki hukutana na dume mara moja tu, na kuanzia muda huo anaweza kuendelea kutaga mayai hadi kufikia mayai 3000 kwa siku wakati wa msimu. Pamoja na taarifa hii ya kushangaza, anaweza kuendelea kutaga mayai kwa miaka mitano..

Thamani ya virutubishi katika royal jelly:
Chakula hiki chenye uwingi wa virutubishi si cha thamani kwa nyuki tu. Kina uwingi wa protini, lipids, glucides, vitamini, homoni, vimeng'enya (enzymes), madini na vitu vyenye sifa ya kuchochea uundwaji wa seli mpya katika mwili wa binadamu. Ingawa baadhi ya elementi katika royal jelly zinapatikana kwa kiwango kidogo sana, bado zinaweza kufanya kazi pamoja na co-enzymes kama vichocheo (catalysts) au zikatumia uwingi wake kufanya kazi kwa pamoja (maana yake matokeo ya kazi ya mkusanyiko wa elemnti ni kubwa kuliko jumla ya matokeo ya kazi ya kila moja). Royal jelly ina uwingi wa protini, vitamini B1, B2, B6, C, E, niacin, pantothenic acid, biotin, inositol na folic acid. Kwa taarifa, ina kiwango cha pantothenic acid ambacho ni mara 17 ya kile kilichomo ndani ya poleni kavu. Ni chakula bora ambacho kimeitwa " liquid nutrient gold". Kapsuli ya Royal Jelly ya Green World ina uhalisi wa asilimia 100 na utendaji kazi wa asilimia 97, mara tatu ya ule wa royal jelly iliyotoka kuvunwa.

Royal Jelly





<<<<< MWANZO